MUZAFFARABAD: Pakistan yakumbuka wahanga wa tetemeko la ardhi
8 Oktoba 2006Matangazo
Rais Pervez Musharraf wa Pakistan na wananchi wenzake wamebakia kimya kwa dakika moja kuadhimisha mwaka mmoja tangu kutokea tetemeko la ardhi lililoua kama watu 75,000 nchini humo.Zaidi ya watu milioni 3.5 wamepoteza makazi yao katika tetemeo hilo la ardhi lililokuwa na nguvu ya 7.6 katika Kipimo cha Richter.