1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu akataa pendekezo la Obama

Martin,Prema/afpe,rtre21 Mei 2011

Rais wa Marekani Barack Obama na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamekutana mjini Washington kuujadili mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/RPGz
President Barack Obama, right, meets with Prime Minister Benjamin Netanyahu, left, of Israel in the Oval Office at the White House in Washington, Friday, May 20, 2011. (AP Photo/Charles Dharapak)
Rais Barack Obama wa Marekani (kulia) na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin NetanyahuPicha: AP

Kufuatia mazungumzo hayo, Obama alikiri kuwa kulikuwepo tofauti za maoni kuhusu njia ya kupata amani katika kanda hiyo na akaongezea kuwa kwa Marekani, usalama wa Israel ni suala lenye umuhimu mkubwa. Mkutano wa viongozi huo umefanyika kufuatia mivutano iliyozuka baada ya Obama hivi karibuni kupendekeza kuwa taifa la Palestina litakaloundwa siku zijazo,liwe chini ya msingi wa mipaka iliyokuwepo kabla ya mwaka 1967.

Netanyahu amepinga vikali pendekezo hilo. Kwa maoni yake, Wapalestina watapaswa kukubali baadhi ya mambo ya kimsingi yaliyokuwa hali halisi.Amesema kuwa Israel ipo tayari kuafikiana ili kupata amani lakini haiwezi kurejea katika mipaka ya mwaka 1967, kwani mipaka hiyo haiwezi kulindwa. Vile vile mipaka hiyo haizingatii mabadiliko ya kijamii yaliyotokea katika kipindi cha miaka 44 iliyopita. Hata hivyo, Netanyahu amesema kuwa ataendelea kushirikiana na Obama kutafuta ufumbuzi wa amani utakaohakikisha usalama wa Israel.