NEW DELHI:India yafanya jaribio la kombora la masafa mafupi
5 Oktoba 2007Matangazo
India imefanya jaribio la kombora la masafa mafupi katika jimbo la mashariki la Orissa.
Hii ni mara ya nne kwa India kufanya jaribio la makombora yake ya masafa mafupi ya aina ya Agni -1 tangu mwaka 2002.
Kombora hilo la Agni- 1 lina uwezo wa kubeba kichwa cha nyuklia chenye uzani wa tani moja na linaweza kupiga umbali wa kilomita 700.
India na nchi jirani yake ya Pakistan mara kwa mara huwa zinatekeleza majaribio ya makombora kwa sharti kwamba zinaarifiana kabla.