1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pendekezo la kutaka kupanua uanachama wa baraza la Usalama

21 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DSIh

NEW YORK:

Ujerumani na Cyprus zimetawanya muswada jaribio ambao unapendekeza kuongeza wanachama wapya wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Hii ndio mara ya kwanza kujaribu kuumaliza mzozo ambao umekuwa unaligubika suala la kupanua baraza hilo.Miongoni mwa mataifa yaliyomstari wa mbele kugombania unachama wa kudumu katika baraza hilo ni Ujerumani,japan,India,Brazil pamoja na nchi ambayo hiajaamuliwa ya Afrika.Wakosoaji wa baraza hilo la wanachama 15 linalohusika na masuala ya kuchunguza usalama na amani dunaini wanasema kuwa, wansema muundo wake umepitwa na wakati na ni lazima ubadili mwelekeo ili kuambatana na wakati wa karne ya 21.Wanadiplomasia wanasema kuwa sasa kuna mwamko mpya wa baraza hilo kuweza kupanuliwa.