1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Bush asema Israel ni taifa la kweli la kidemokrasia.

Mohamed Dahman14 Mei 2008

Rais George Bush wa Marekani ameanza ziara ya masaa 48 kwa Israel leo hii kwa kuyakinisha ushirika wake wa kudumu na taifa hilo.

https://p.dw.com/p/DzwN
George W. Bush katikati akikumbatiwa na Waziri Mkuu wa Israeli Ehud Olmert wakati Rais Shimon Peres wa Israel akiangalia mara tu baada ya Bush kuwasilia katikja uwanja wa ndege wa Ben Gurio leo hii.Picha: AP

Ziara ya Bush Mashariki ya Kati inakita katika maadhimisho ya miaka 60 tokea kuundwa kwa taifa la Israel na inalenga kuimarisha mpango wa amani Mashariki ya Kati wakati umwagaji damu ukiendelea.

Akiliita taifa la Israel kuwa taifa la kidemokrasia ya kweli Bush amemuambia Rais wa Israel Shimon Perez mjini Jerusalem kwamba anatuhumu iwapo mtu ataangalia nyuma miaka 60 iliopita ana mashaka iwapo watu wangeliweza kutabiri kuwepo kwa Israel ya kisasa.

Amekaririwa akisema kile kilichotokea hapo kinaweza kutokea mahala popote pale.

Bush anaitembelea Israel wakati nchi hiyo ikisheherekea miaka 60 ya kujitangazia kuanzishwa kwa taifa hilo hapo tarehe 14 mwezi wa Mei mwaka 1948.Bush anatazamiwa kuhutubia mkutano wa kimataifa kuadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwa taifa hilo mkutano ambao utahudhuriwa na viongozi muhimu duniani ukiwa chini ya uwenyeji wa Rais Perez leo usiku kadhalika hapo kesho mchana atalihutubia bunge la Israel.

Katika mikutano yake kadhaa na viongozi wa Israel kabla ya kuondoka kwake hapo Ijumaa Bush atataarifiwa juu ya mchakato mgumu wa amani kati ya Israel na Wapalestina ambao chini ya usimamizi wake ulifufuliwa mwaka jana kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka saba.

Tafauti na ziara yake ya kwanza hapo mwezi wa Januari Bush hatokwenda Ramallah lakini atajulishwa juu ya mazungunzo hayo na upande wa Wapalestina katika mkutano na Rais Mahmoud Abbas huko Sharm el - Sheikh nchini Misri hapo Jumamosi na Jumapili.

Bush alipewa makaribisho mazuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ben Gurion mapema leo hii.

Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert ameuita ushirika wa Israel na Marekani kuwa mojawapo ya nguzo muhimu za usalama wao wa taifa.

Wakati Israel ikiendelea na sherehe zake zilizoanza wiki iliopita Wapalestina katika maeneo yote ya Gaza na Ukingo wa Magharibi wameanza kumbukumbu ya miaka 60 ya vita vya Israel na Waarabu vya mwaka 1948- 1949 ambavyo vilizuka kufuatia kuundwa kwa taifa hilo la Israel.

Katika vita hivyo ambapo mamia kwa maelfu ya wakimbizi wa Wapalestina walikimbia makaazi yao katika kile ambacho hivi sasa ndio Israel kwa wao inajulikana kuwa ni Nakba kwa Kiarabu ikimaanisha balaa.

Huko Gaza afisa mwandamizi wa kundi la Hamas Mahmoud al Zahar ameuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba kundi lake katu halltoitambua Israel

na kwamba Israel iko siku itatoweka na wananchi wa Palestina wataendelea kuikombowa ardhi yao kikamilifu.

Lakini licha ya umwagaji damu wa Gaza na mabishano makali juu ya unjenzi wa makaazi ya walowezi wa Kiyahudi Bush amesema kabla ya kuanza kwa ziara yake hiyo ya Mashariki ya Kati ambayo pia itamfikisha Msiri na Saudi Arabia kwamba anaamini makubaliano ya amani yataweza kufikiwa kabla ya kumalizika kwa muda wake madarakani hapo mwezi wa Januari mwaka 2009.