1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Smith afariki dunia.

21 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQ2o

Harare. Kiongozi wa zamani wa utawala wa Wazungu wachache nchini Zimbabwe, Ian Smith amefariki dunia nchini Afrika kusini akiwa na umri wa miaka 88. Katika mwaka 1965 Smith aliongoza Wazungu karibu laki mbili na nusu wakati huo nchi hiyo ikiitwa Rhodesia na kuitangaza nchi hiyo kuwa huru kutoka Uingereza kuliko kukubali pendekezo la utawala wa Waafrika waliowengi. Alibaki madarakani kama waziri mkuu hadi pale vita vya wapiganaji wa chini kwa chini vilipomlazimisha kukubali makubaliano ya kusitisha mapigano na kupatikana suluhisho la kisiasa mwaka 1979.

Uchaguzi ulifanyika mwaka uliofuata, wakati Rhodesia ilipobadishwa jina na kuitwa Zimbabwe katika utawala wa Waafrika waliowengi, na Robert Gabriel Mugabe kuwa waziri mkuu. Smith aliendelea kumpinga Mugabe, hata baada ya sheria ya kuwa na viti maalum vya bunge vilivyotengwa kwa ajili ya wazungu kuondolewa katika mwaka 1987.