1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran kupunguza ushirikiano wake na Shirika la Umoja wa Mataifa la nguvu za Atomiki.

27 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfq

Bunge la Iran limepiga kura kuitaka serikali kuchunguza upya uhusiano wake na shirika la Umoja wa Mataifa la nguvu za Atomiki.

Hatua hiyo huenda ikaifanya Iran kupunguza ushirikiano kati yake na shirika hilo linalochunguza mradi wake wa kinyuklia.

Kura hiyo imepigwa siku nne baada ya baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuamua kuiwekea Iran vikwazo vichache kutokana na hatua yake ya kukataa kukomesha urutubishaji wa madini ya yurani.

Halmashauri ya magavana wa shirika hilo itakutaka mwezi ujao kujadili jinsi ya kutekeleza vikwazo hivyo dhidi ya Iran.

Ingawa shirika hilo limefanya uchunguzi kwa takriban miak minne, halijaweza kuthibitisha iwapo mradi wa kinyuklia wa Iran unaweza kutumiwa kwa silaha za nyuklia.

Shirika hilo lilianza uchunguzi mara baada ya kundi la upinzani kufichua habari za mradi huo wa siri wa kinyuklia.