1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

THE HAGUE: Uholanzi yaukosoa mpango wa rais Bush

12 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbH

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Uholanzi, Ben Bot ameukosoa mpango mpya wa rais George W Bush wa Marekani wa kutaka kupeleka wanajeshi zaidi nchini Irak.

Bot amewaambia waandishi wa habari mjini The Hague leo kwamba wanajeshi zaidi wamekuwa wakipelekwa Irak kwa miaka kadhaa bila mafanikio yoyote.

Ben Bot amesema rais Bush hakuzijumuisha nchi jirani na Irak katika mpango wake wa kuliimarisha eneo zima.

Waziri Bot amesema Uholanzi itaendelda kuwasiliana na Syria na Lebanon. Uholanzi ilipeleka wanajeshi wake 1,400 kusini mwa Irak baada ya uvamizi wa mwaka wa 2003 ulioongozwa na Marekani. Hata hivyo wanajeshi hao walirejea nyumbani mnamo mwaka wa 2005 baada ya wadachi kupinga uamuzi huo wa serikali.

Wabunge wa Marekani wameukosoa pia mpango wa rais Bush. Mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulikia mahusiano ya kigeni wa chama cha Democratic, Joe Biden, ameuleza mpango wa rais Bush kuwa kosa kubwa. Mbunge Joe Hagel wa chama cha Republican cha rais Bush, ameeleza pia msimamo kama huo.