1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Robert Zoellick ateuliwa kuwa rais mpya wa benki ya dunia

30 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwV

Rais George W Bush wa Marekani amemteua Robert Zoellick, mjumbe wa zamani wa biashara wa Marekani, kuwa rais mpya wa benki ya dunia.

Kwa mujibu wa afisa katika utawala wa rais Bush ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema uteuzi wa bwana Robert Zoellick utatangazwa wakati wowote kutoka sasa.

Zoellick atachukua nafasi ya rais wa zamani wa benki ya dunia, Paul Wolfowitz, atakayeondoka rasmi madarakani ifikapo Juni 30.

Wolfowitz alipatikana na makosa ya kuvunja sheria za benki ya dunia kwa kumpandisha cheo na kumuongezea msharaka mpenzi wake, Shaha Riza, ambaye ni mfanyakazi wa benki hiyo.

Uteuzi wa bwana Robert Zoellick kuchukua nafasi ya Paul Wolfowitz unatarajiwa kuidhinishwa na bodi ya magavana 24 wa benki ya dunia.

Katika taarifa yake iliyotolewa hapo jana bodi hiyo haiukusema lolote kuhusu uteuzi wa bwana Zoellick, lakini ikadokeza mkurugenzi yeyote ana haki ya kupendekeza mtu atakayechukua wadhifa wa urais wa benki ya dunia.