1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yangoon. Gambari ahutubia baraza la usalama.

14 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1a

Mjumbe wa umoja wa mataifa Ibrahim Gambari amelihutubia baraza la usalama la umoja wa mataifa , kufuatia ujumbe wake wa siku sita nchini Burma. Ameliambia baraza hilo kuwa amepata matumaini na hatua muhimu zilizochukuliwa na utawala wa kijeshi wa nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na kuondoa amri ya kutotembea usiku, iliyowekwa wakati wa maandamano ya kuipinga serikali, na kuachiliwa kwa kiasi cha watu 2,700 waliokamatwa ikiwa ni pamoja na wafungwa wa kisiasa. Lakini ameeleza pia kuwa utawala wa Burma haujaweza bado kutoa uhakikisho kuwa utaondoa vikwazo dhidi ya kiongozi wa upinzani, Aung San Suu Kyi, ambaye amekuwa kizuizini nyumbani kwake kwa zaidi ya miaka 18. Pia ameeleza wasi wasi wake juu ya ripoti zinazozidi kupatikana za kuendewa kinyume haki za binadamu. Wakati Gambari amelenga katika mambo mazuri ya ziara yake , balozi wa Uingereza John Sawers amesema kuwa udhibiti katika ziara ya Gambari unaonyesha kuwa mwelekeo wa serikali katika ziara hiyo haukufikia matarajio ya baraza la usalama.