1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZURICH: Blatter achaguliwa tena rais wa FIFA

1 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBwD

Sepp Blatter amechaguliwa kwa mara ya tatu kama rais wa shirika linalosimamia soka duniani-FIFA.Blatter alikuwa mgombea pekee wa cheo hicho cha kipindi cha miaka minne.Upigaji kura ulifanywa katika Baraza la FIFA mjini Zurich, Uswisi.Blatter alie raia wa Kiswisi alichaguliwa mara ya kwanza kama rais wa FIFA mwaka 1998.Kwa upande mwingine Franz Beckenbauer wa Ujerumani amechaguliwa mwanachama wa Ulaya katika kamati utendaji ya FIFA.