1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la mawaziri Misri latangaza kujiuzulu

22 Novemba 2011

Baraza la mawaziri nchini Misri limewasilisha pendekezo la kujiuzulu kuiongoza nchi hiyo kwa utawala wa kijeshi wakati kukiwa na maandamano ya umma katika maeneo ya mji mkuu wa Cairo na kwengineko.

https://p.dw.com/p/13EeK
Waandamanaji mjini CairoPicha: picture-alliance/dpa

Katika kauli yake aliyowasilisha kupitia televisheni ya taifa, msemaji wa serikali alisema serikali imekwishwa wasilisha taarifa ya kujiuzulu, lakini itaendelea na majukumu yake ya kila siku nchini humo katika kukabiliana na wakati mgumu.

Hata hivyo kuna taarifa zenye utata juu ya mapokezi ya baraza la kijeshi la nchi hiyo kuhusu taarifa hiyo. Hatua hiyo inafuatia vurugu za siku tatu nchini humo kati ya vikosi vya usalama vya Misri na raia wanaoandamana katika uwanja wa Tahrir.

Zaidi ya watu 20 wameuwawa katika machafuko hayo. Mapema jana wanadiplomasia 140 wa Kimisri waliopo katika wizara za kigeni na balozi nje ya taifa hilo wametoa tamko lililotaka vikosi vya usalama viache kutumia nguvu dhidi ya raia wanaoandamana kwa amani.

Mwandishi: Sudi Mnette

Mhariri: Josephat Charo