1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michuano ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za kombe la ubingwa wa mataifa ya Ulaya leo.

12 Septemba 2011

Ujerumani inatarajiwa kuwa timu ya kwanza kufanikiwa, pindi itaibwaga Austria mjini Gelsenkirechen.

https://p.dw.com/p/RjRP
Kocha wa Ujerumani Joachim Loew akitoa agizo katika moja wapo ya mechi zilizopita.Picha: AP

Ujerumani sawa na Uhispania na Uholanzi, hadi sasa imecheza mechi zake za kombe la ubingwa wa mataifa ya Ulaya, mashindano yatakayofanyika mwakani yakiandaliwa kwa ubia nchini Poland na Ukraine. Pindi Ujerumani itashinda jioni hii ya leo basi utakua ushindi wake wa nane mfululizo.Hata kama ikishindwa, kikosi hicho cha kocha Joachim Loew bado kitaweza kusonga mbele pindi Uturuki itashindwa kutamba mbele ya Kazakhstan.

Ujerumani ilioshindwa na Uhispania katiaka fainali ya kombe la Ualaya 2008 ilipotandikwa bao moja kwa bila mjini Vienna, ina uongoza kwa ufungaji mabao mengi zaidi, ikiwa na magoli 22,moja la ziada kuliko Uholanzi. Miroslav Klose ameuona wavu mara nane na anahitaji mabao 7 tu kuifikia rekodi ya Gerd Muller ya mabao 68.Kocha Loew amesema wanaifahamu vizuri Austria na hivyo watakua makini.

Kwa upande wa Uturuki iliyo nafasi ya tatu , ina nafasi nzuri kimsingi ya kuwa nyuma ya Ujerumani. Italia katika kundi C inachuana na visiwa vya Faroe mechi ambayo ushindi kwa wataliani linaonekana ni jambo la dhahiri. Uhoalanzi huenda ikahitaji kusubiri zaidi kabla ya kusherehekea mafanikio yake katika kundi E.

Wadachi hao awana pambano rahisi nyumbani dhidi ya San Marino, lakini Sweden inayoiandama ina kasoro ya pointi 3 tu na italazimika kutoa shinikizo katika mchuano wake na Hungary inayoshika nafasi ya tatu.

Timu ya Ufaransa ya kocha Laurent Blanc iko Albania. Ufaransa ambayo imeshinda mechi 11 za kurafiki kabla ya kufungwa bao 1-0 ana Belarus katika mechi ya mashindano ya kombe la Ulaya bila shaka itataka kuhakikisha inaibuka na ushindsi leo.

Katika kundi H, Ureno yenye pointi sawa na Norway na Denamark lakini ikiongoza kwa wingi wa goli moja tu, inamenyana na Cyprus mjini Nikosia.Uingereza inacheza na Montenegro na katika mechi nyengine ya kundi G Bulgaria itakua ugenini kupambana na Wales . Ireland katika kundi B itatoana jasho na Slovakia katika mechi kati ya timu mbili zinazogawana uongozi.

Urusi ambayo pia ina ponti 13 kutokana na mechi 6 ilizocheza hadi sasa inakaribishwa na Macedonia , wakati katika mechi za kundi F, Israel ilioko nafasi ya tatu na ikiwa imecheza mechi moja ya zaidi inaikaribisha Ugiriki mjini Tel Aviv.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman /ap

Mhariri: Josephat Charo