1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tetemeko la ardhi latokea Indonesia

7 Januari 2008
https://p.dw.com/p/ClPE

JAKARTA:

Tetemeko kubwa la ardhi limelitikisha eneo la mashariki ya Indonesia, hata hivyo hakuna hatari ya kutokea Tsunami.

Tetemeko ambalo kipimo chake kimetajwa kama 6.2 liliutikisa mkoa wa Papua na kuharibu nyumba kadhaa na pia kuleta hofu kwa wakazi wa eneo hilo lakini hakukutokea vifo.

Kituo cha utafiti wa jiolojia cha Marekani kimesema kuwa tetemeko hilo limeeneoa katika umbali wa kilomita 35 tu na kitovu chake kimerikodiwa kuwa kilomita nane kaskazini mwa mji wa mwambao wa Manokwari katika mkoa wa Papua magharibi.

Indonesia imekaa katika kile kinachoweza kuelezwa kama-duara ya moto ya Pasifiki,eneo ambalo ni hai mno kwa mitetemeko ya ardhi ya kila mara.