1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

10 wafa katika bomu la kujitoa mhanga Iraq

2 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CjA4

BAGHDAD:

Watu 10 wameuawa na wengine nane kujeruhiwa katika bomu la kujitoa mhanga lililotokea mjini Baghdad jumatano.

Polisi wanasema mtu aliejilipua alikuwa mwanamke ambae alijilipua katika kituo cha ukaguzi cha watu waliojitolea kufanya ulinzi katika mtaa mmoja baquba katika mkoa wa Diyala.Polisi inasema wengi wahanga walikuwa ni walinzi waliojitolea kufanya doria.Washika doria hao wako katika mtaa wa Kissuni na wanalipwa kwa kazi yao na wamarekani.