Matukio ya kisiasa

Matukio ya Afrika

Masuala ya jamii

Michezo

Habari kwa lugha ya Kiingereza

Tazama vidio 01:18
Sasa moja kwa moja
dakika (0)
13.12.2018 | 13.12.2018

Mashini za kupigia kura zateketezwa kwa moto Kinshasa

Hatari ya kukosa maarifa – Namna viongozi wa Afrika walivyoshughulikia Ukimwi

Ukaidi wa kutisha.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki (1999-2008) atakumbukwa na historia kama kiongozi wa mwanzo kabisa wa Afrika aliyekataa uwepo wa Ukimwi. Licha ya ushahidi wote wa kisayansi alishikilia msimamo wake kuwa virusi vya HIV havisababishi Ukimwi. Aliwaelekeza maafisa wake wa afya kuutokomeza Ukimwi kwa dawa za miti shamba. Watu 300,000 wanahofiwa walikufa kutokana na msimamo huo wa Mbeki.

Hatari ya kukosa maarifa – Namna viongozi wa Afrika walivyoshughulikia Ukimwi

Rais kama mganga wa kienyeji

Mwaka 2007 rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh (1996 - 2017) aliwalazimisha wagonjwa wa Ukimwi kupatiwa tiba aliyoibuni mwenyewe. Ilikuja kugundulika kuwa tiba hiyo ilikuwa ni mchanganyiko wa miti shamba; idadi ya watu isiyojulikana walifariki dunia. Jammeh, aliyedai kuwa na nguvu za mizimu na miujiza, ni kiongozi wa kwanza wa Afrika kushtakiwa kwa kukiuka haki za watu wenye virusi vya Ukimwi.

Hatari ya kukosa maarifa – Namna viongozi wa Afrika walivyoshughulikia Ukimwi

'Wewe oga tu'

Rais mwingine wa zamani wa Afrika Kusini aliyezua gumzo juu ya namna alivyoushughulikia Ukimwi ni Jacob Zuma. Baada ya kushtakiwa kumbaka mwanamke aliyekuwa na virusi vya Ukimwi mwaka 2006, Zuma alisema asingeweza kuwa muathirika licha ya kutotumia kondomu, kwa sababu "alioga baada ya kitendo hicho." Mwaka 2010 Zuma alifichua hali yake ya kiafya ya kutokuwa na Ukimwi ili kuepuka unyanyapaa.

Hatari ya kukosa maarifa – Namna viongozi wa Afrika walivyoshughulikia Ukimwi

Bila kondomu?

Rais wa Uganda Yoweri Museveni alitumia muda mrefu kabla ya kujiunga na vita dhidi ya Ukimwi. Mwaka 2004, wakati wa mkutano wa kimataifa kuhusu Ukimwi huko Thailand, alipuuza ufanisi wa kutumia kondomu, akisema zinakwenda kinyume na tamaduni za kiafrika. Alisema "sidhani kama wote duniani tunaweza kuwa wavaa kondomu." Matamshi yake yaliwafanya washiriki wa mkutano kuangua kicheko.

Hatari ya kukosa maarifa – Namna viongozi wa Afrika walivyoshughulikia Ukimwi

Kodi ya kufadhili matibabu

Baadhi ya hatua zilizochukuliwa na marais wa Afrika kupambana na Ukimwi hazikufanikiwa. Kodi iliyoanzishwa mwaka 1999 na rais wa zamani wa Zimbambwe Robert Mugabe kusaidia yatima na wagonjwa wa Ukimwi iligomewa na raia. Kodi hiyo bado ipo hadi leo. Mwaka 2004 Mugabe alisema familia yake ni miongoni mwa wahanga wa maradhi hayo na kuutaja Ukimwi kuwa janga baya kabisa linaloikabili nchi hiyo.

Hatari ya kukosa maarifa – Namna viongozi wa Afrika walivyoshughulikia Ukimwi

Mfano wa kuigwa

Hofu ya athari kwa chumi za mataifa yao kama sekta ya Utalii ni moja ya sababu zilizowafanya viongozi wa Afrika kujizuia kukubali kitisho cha Ukimwi. Lakini rais Kenneth Kaunda wa Zambia alitangaza mapema mwaka 1987 kwamba mtoto wake wa kiume alifariki kwa Ukimwi. Mwaka 2002 alikuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kupima Ukimwi hadharani. Hadi leo bado anapambana dhidi ya Ukimwi.

Hatari ya kukosa maarifa – Namna viongozi wa Afrika walivyoshughulikia Ukimwi

Jaribio la kutaka kupima ukimwi iwe lazima.

Mapambano dhidi ya Ukimwi kutoka kwa mrithi wa Kaunda, rais Edgar Lungu yalikutana na vizingiti alipojaribu kutaka upimaji wa Ukimwi uwe lazima nchini Zambia. Lungu alisema mnamo 2016 kuwa sera hiyo haina majadiliano.Ukosoaji mkubwa wa ndani na nje ya nchi ulimlazimisha kusalimu amri hasa baada ya Shirika la Afya Duniani WHO kusema kuwa upimaji wa lazima unaongeza unyanyapaa kwa walioathirika.

Hatari ya kukosa maarifa – Namna viongozi wa Afrika walivyoshughulikia Ukimwi

Kinara wa kampeni ya Afrika bila Ukimwi

Baada ya kuondoka madarakani rais wa zamani wa Botswana, Festus Mogae, (1998-2008), alianzisha kampeni ya "kizazi bila Ukimwi" ambayo iliwaleta pamoja marais kadhaa wa zamani wa Afrika na watu wengine mashuhuri kupambana na janga hilo. Wanatumai kuwa uzoefu na ushawishi wao unatasaidia kuongeza msukumo kwa serikali na washirika wengine kuwekeza zaidi katika kupambana na Ukimwi.

Albanian Shqip

Amharic አማርኛ

Arabic العربية

Bengali বাংলা

Bosnian B/H/S

Bulgarian Български

Chinese (Simplified) 简

Chinese (Traditional) 繁

Croatian Hrvatski

Dari دری

English English

French Français

German Deutsch

Greek Ελληνικά

Hausa Hausa

Hindi हिन्दी

Indonesian Indonesia

Kiswahili Kiswahili

Macedonian Македонски

Pashto پښتو

Persian فارسی

Polish Polski

Portuguese Português para África

Portuguese Português do Brasil

Romanian Română

Russian Русский

Serbian Српски/Srpski

Spanish Español

Turkish Türkçe

Ukrainian Українська

Urdu اردو