1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

40 wauwawa Syria

26 Oktoba 2013

Bomu lililotegwa katika gari nje ya msikiti karibu na mji wa Damascus limewaua watu 40 Ijumaa(25.10.20213),wakati afisa wa Umoja wa Mataifa ameeleza wasi wasi mkubwa kuhusu mamia ya watu ambao wamezingirwa.

https://p.dw.com/p/1A6U1
A handout picture made available by Syrian news agency (SANA) shows a Syrian soldier carrying a wounded child to receivE first aid at Al Muwasat Hospital in Damascus, after injured at the site of a car bomb attack near Osama bin Zaid Mosque in Souk Wadi Barada in Rural Damascus, Syria, 25 October 2013. An official source told SANA that the explosion of the car led to the deaths of terrorists inside their car, and three citizens killed including a child, and 30 wounded, most of them in critical condition. As victims were being taken to the hospital, one of the injured people said, 'the explosion occurred before the end of Friday prayers and led to the collapse of the entrances of the mosque, damaging several shops and vehicles at the scene'. dpa/EPA/SANA HANDOUT /eingest. sc
Shambulio mjini Damascus , wamo watoto waliofarikiPicha: dpa

Mamia ya watu wamejeruhiwa katika shambulio la bomu lililotegwa katika gari katika mji wa Suq Wadi Barada, shirika lenye makao yake makuu nchini Uingereza la kuangalia haki za binadamu nchini Syria limesema, na ambalo linategemea mtandao wa wanaharakati na watu wengine ambao wameshuhudia matukio.

Serikali ya Syria na upinzani wamelaumiana kutokana na mauaji hayo. Suq Wadi Barada ni mji ambao unadhibitiwa na waasi na umezingirwa na majeshi tiifu ya utawala wa rais Bashar al-Assad.

Turkish soldiers take position in the southern border town of Akcakale on October 4, 2012. Turkish artillery hit targets near Syria's Tel Abyad border town for a second day on Thursday, killing several Syrian soldiers according to activists and security sources, after a mortar bomb fired from the area killed five Turkish civilians. Turkey's government said 'aggressive action' against its territory by Syria's military had become a serious threat to its national security and sought parliamentary approval for the deployment of Turkish troops beyond its borders. AFP PHOTO/BULENT KILIC (Photo credit should read BULENT KILIC/AFP/GettyImages)
Wanajeshi wa kulinda amaniPicha: Bulent Kilic/AFP/GettyImages

"Idadi ya watu waliouwawa kutokana na shambulio la bomu lililotegwa katika gari ambalo liliripuka baada ya sala ya Ijumaa katika mji wa Suq Wadi Barada imepanda hadi watu 40, ikiwa ni pamoja na watoto na wanawake," limesema shirika hilo la uchunguzi wa haki za binadamu.

"Idadi ya waliofariki huenda ikapanda kwasababu kuna watu kadha ambao wamejeruhiwa, wengi wao wako katika hali mbaya sana,"Limeongeza.

Magaidi wanahusika

Shirika la habari la Syria SANA , hapo kabla liliripoti kuhusu mripuko huo, na kulaumu kile lilichokiita kuwa ni "magaidi", neno linalotumiwa na utawala wa Assad kuwaelezea wapiganaji wanaojaribu kuuondoa utawala wake. Shirika la habari la SANA limesema "gari hiyo iliripuka wakati magaidi wakiwa wanaweka miripuko ndani ya gari hiyo ".

Kundi la muungano wa kitaifa wa upinzani wakati huo huo limeilaumu serikali ya Assad kwa mauaji yaliyosababishwa na kile ilichosema kuwa ni miripuko miwili ya mabomu yaliyotegwa katika magari yaliyowekwa nje ya msikiti wa Osama bin Zeid mjini Suq Wadi Barada. Mashambulio ya mabomu yaliyotegwa katika magari yamekuwa yakitokea mara kwa mara nchini Syria katika miezi ya hivi karibuni, na kuuwa watu kadha nchini humo.

Syrian in Zaatari, Flüchtlingslager in Jordanien Place and date: 2012 Mafraq - Jordan Copyright: Mohamad AL Anasweh - DW via Hasan Hussain, DW Arabisch
Wakimbizi wa Syria nchini JordanPicha: DW

Televisheni ya Syria wakati huo huo imeripoti kuwa Abu Mohammed al-Jawlani , kiongozi wa kundi la al-Nusra Front , kundi la waasi lenye nguvu la Waislamu wanaofuata nadharia za jihad ambalo linamahusiano na al-Qaeda, ameuwawa kaskazini magharibi ya jimbo la Latakia, lakini kundi hilo baadaye limesema yuko katika hali nzuri.

Ghasia zaongezeka

Katika tukio jingine la ghasia shambulio la kushtukiza mashariki ya Damascus limewauwa waasi 24, limesema shirika hilo la kuangalia haki za binadamu nchini Syria , wakati shirika la habari la SANA limesema idadi ya waasi waliouwawa ni 40.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa na wa Marekani wameeleza wasi wasi wao kuhusiana na eneo la Ghouta ya mashariki pamoja na maeneo mengine ya vitongoji vya mji mkuu Damascus ambavyo vimezingirwa, kufuatia ripoti kuwa kuna uhaba mkubwa wa chakula na kiwango ambacho kinaongezeka cha utapia mlo.

British Valerie Amos, United Nations Under-Secretary-General for Humanitarian Affairs and Emergency Relief Coordinator, launchs the Humanitarian Appeal 2011, during a press conference at the European headquarters of the United Nations in Geneva, Switzerland, 30 November 2010. EPA/SALVATORE DI NOLFI +++(c) dpa - Bildfunk+++
Mkuu wa idara ya misaada ya dharura ya Umoja wa mataifa Valerie AmosPicha: picture-alliance/dpa

Mkuu wa idara ya Umoja wa Mataifa inayotoa misaada ya kiutu Valerie Amos siku ya Ijumaa (25.10.2013) amelitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuweka mbinyo dhidi ya serikali ya Syria kuruhusu misaada kuingia katika eneo hilo ambalo lina wakaazi raia milioni 2.5 ambao wamekwama kutokana na mzozo huo.

Amos ameliambia baraza hilo lenye wanachama 15 kuwa "maneno , bila ya kuwa na uwezo wa kutoa msukumo, hayawezi kutengeneza picha ya madhila na mateso yanayotokea nchini Syria.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Iddi Ssessanga