1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

5 wauawa katika shambulio la bomu Pakistan

18 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CtM9

PESHAWAR:

Nchini Pakistan watu wapatao watano wameuawa katika shambulio ambalo linaaaminiwa kuwa la kujitoa mhanga kwenye msikiti wa Kishia katika mji wa Peshawar ulioko kaskazini magharibi mwa nchini hiyo.

Watu 20 wamejeruhiwa katika mlipuko huo.Vyombo vya habari katika eneo hilo,vimeripoti kuwa msikiti wa Imam Bargah Qasim Baig ulikuwa umejaaa waumini wakati wa shambulio hilo. Afisa wa polisi amesema kuwa bomu lilipuka wakati askari polisi walipomsimamisha mtu mmoja, aliekuwa anataka kuingia katika msikiti huo, ili kumfanyia upekuzi.Pakistan imekumbwa na milipuko kadhaa ya mabomu baada ya vikosi vya usalama kuvamia Msikiti mwekundu wa Islamabad mwezi julai mwaka jana.