1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACCRA: Rais wa Ujerumani, Horst Koehler, atoa wito wa ushirkiano wa Afrika na Ulaya kwa amani ya Somalia.

13 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCb1

Rais wa Ujerumani, Horst Köhler ametoa wito kwa nchi za Afrika kushirikiana na Ulaya katika harakati za kuhakikisha amani nchini Somalia na maeneo mengine yenye mizozo barani humo.

Rais Horst Köhler alisema hayo kwenye mkutano kati yake na Rais wa Ghana, John Kuffuor mjini Accra.

Rais huyo wa Ujerumani yumo katika ziara rasmi ya siku nne nchini Ghana.

Rais John Kuffuor ameipongeza Ujerumani kwa ufadhili wa maendeleo nchini mwake.

Mwaka uliopita Ujerumani ilitoa ufadhili wa maendeleo wa zaidi ya Yuro bilioni moja kwa Ghana.