1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACCRA:Afrika waungana na Uingereza kuadhimisha miaka 200 kuzuia utumwa

26 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFG

Waafrika waliungana na Uingereza katika kuadhimisha miaka 200 toka Uingereza ilipopiga marufuku biashara ya utumwa.

Watu wa kizazi kilichotokana na utumwa pamoja na wakuu mbalimbali walikusanyika katika ngome ya zamani ya watumwa ya Elmina huko Ghana kukumbuka zaidi ya waafrika millioni 10 waliyouzwa katika sehemu mbalimbali huko Marekani.

Rais wa Ghana ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, John Kufour, katika hotuba yake alisema biashara ya utumwa si ubinaadamu.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Uingereza Tony Blair alielezea kile alichosema masikitiko na majuto makubwa kwa Uingereza kuhusika katika biashara ya utumwa.