1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Addis Ababa. Kampuni ya Malaysia kuendeleza machimbo ya gesi.

13 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZd

Ethiopia imetia saini makubaliano yanayoiruhusu kampuni ya Malaysia, ya Petronas kuendeleza gesi ya ardhini katika jimbo lake la Ogaden ambako waasi wameionya kampuni hiyo kutofanya hivyo.

Maafisa wizara ya madini na nishati wamesema kuwa makubaliano yaliyotiwa saini kati ya Ethiopia na kampuni la Petronas yanalenga katika uendelezaji na uuzaji wa gesi inayopatikana katika machimbo ya Kalub na Hilal katika jimbo la Ogaden.

Maafisa hao wamesema kuwa kiasi cha dola milioni 1.9 kitalipwa kama gharama za uendeshaji, lakini hawakutoa gharama za mradi mzima. Waziri wa madini na nishati wa Ethiopia Alemayeu Tegenu alitia saini makubaliano hayo na Petronas mjini Kuala Lumpur mwezi uliopita baada ya kampuni hilo la Malaysia kushinda tenda kwa ajili ya gesi ya iliyopo katika maeneo ya Kalub na Hilal.