1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA:Mkutano wa maridhiano Somalia wakhairishwa

3 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5I

Mkutano wa maridhiano ya makundi yanayopingana nchini Somalia uliokuwa umepangiwa kufanyika mei 16 umehairishwa kwa mwezi mmoja.

Hayo yametangazwa na balozi wa Somalia nchini Ethiopia Abdikarin Farah ambaye amesema hatua hiyo imechukuliwa kwa kuwa hakuna fedha za kugharamia mkutano huo.

Jumuiya ya kimataifa ilitarajiwa kutoa fedha za kugharamia lakini hadi sasa hakuna chochote kilichotolewa.

Mkutano huo ulipangiwa kuwahusisha watu kiasi cha 3000 kutoka nchini Somalia na nje.