1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AFCON. Ghana yamtimuwa kocha timu ya taifa

Zainab Aziz
24 Januari 2024

Kocha wa timu ya taifa ya Ghana, Chris Hughton, ametimuliwa baada ya timu hiyo kutolewa mapema kwenye mashindano ya kugombea ubingwa wa kandanda barani Afrika (AFCON) yanayoendelea nchini Ivory Coast.

https://p.dw.com/p/4bdAr
Ghana, Comoro, CAN
Kipa wa Ghana Abdul Manaf Nurudeen (kulia) akiwania mpira na mshambuliaji wa Comoro, Said Bakari kwenye michuano ya CAN 2021.Picha: DANIEL B. OLOMO/AFP/Getty Images

Taarifa hiyo imetolewa na Shirikisho la Kandanda la Ghana, ikisema kuwa baraza la uongozi pia limeamua kukivunja kikosi cha ufundi cha timu hiyo.

Kocha Chris Hughton amefukuzwa baada ya timu ya Cameroon kuilaza Gambia mabao matatu kwa mawili na hivyo kuinyima Ghana fursa ya kusonga mbele kwenye dimba la  timu 16.

Timu hiyo ya Black Stars ilishindwa kusonga mbele baada ya kutoka sare ya 2-2 na Msumbiji Jumatatu iliyopita.

Shirikisho la Kandanda la Ghana limesema katika siku za hivi karibuni litatoa mwelekeo juu ya mustakabali wa timu hiyo ya taifa ya Ghana.