1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AfDB kutoa Dola Milioni 232.5 kwa ujenzi wa barabara za Tanzania na Kenya

19 Aprili 2013

Kenya na Tanzania kufaidika kwa ujenzi wa barabara ya Kilomita 157.5 kutoka Arusha kwenda Holili Tanzania na Taveta kwenda Voi Kenya ambayo inajengwa kwa mkopo kutoka Benki ya maedeleo ya Afrika AfDBhi

https://p.dw.com/p/18Jdo

Mkopo huo wa Dola Milioni 232.5 umethibitishwa na Benki ya maendeleo ya Afrika AFDB,katika kufaninkisha mradi wa barabara hiyo ili kurahisisha huduma za usafiri na muingiliano wa kimasoko wa nchi za umoja  wa Afrika Mashiriki.

Uluguru Mountains bei Morogoro – Tansania
Barabara nchini TanzaniaPicha: Sascha Quaiser

Mkurugenzi wa Benki ya maendeleo ya Afrika AFDB kanda ya Afrika ya Mashariki, Gabriel Negatu, amethibitisha mkopo huo na kusema kuwa ujenzi wa barabara hiyo tayari ulikuwa katika mkakati wa kanda ya Muingiliano wa  Afrika Maashariki RISP wa mwaka 2011-2015.

''Jumuiya Afrika Mashariki inahitaji kuimarisha miundombinu ya usafiri katika kanda hii,ili kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na ,pango wa maendeleo ya jamii,na kuvutia utalii na muingiliano wa kijamii katika kanda hiyo wakati huo huo kurahisisha  biashara katika mipaka hiyo na biashara za kimataiafa''Amesema Gabriel Nigatu.

Katika mradi huo,Serikali ya Kenya itapokea mkopo wa Dola za Marekani milioni 113.3 katika mkopo waote wa milioni 232.5  unaotolewa na Benki hiyo,huku Tanzania itapokea kiasi cha Dola  milioni 120,huku Banki hiyo ikichangia asilimia 89.1 ya gharama za mradi wote.

Ujenzi huo ambao unadhaminiwa na serikali ya Kenya na Tanzania unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka 2018 ambapo serikali zote mbili kwa zimechangiua kiasi cha Dola milioni 15.6 na Dola milioni 12.3,huku mfuko wa biashara wa Afrika ukichangia kiasi cha Dola asilimia 0.17 milinio,kwa ajili ya kuandaa miundombinu ya biashara katika eneo mpaka wa Namanga,ikiwa jumla ya ghrama zote za mradi huo Dola milioni 262.2.

Chemba Muhimu ya biashara

Barabara ya Arusha-Holili na Taveta-Voi ni chemba muhimu ya usafiri katika ukanda wa Afrika Mashariki, ambayo inaunganisha  Chemba yaKaskazini katika eno la Voi kwenda Chemba ya Kati  kupitia mpaka muhimu eneo la Holili-Taveta  kutokezea Arusha,Babati hadi Dodoma na Singida. Mradi huo utawahusisha wafanyakazi wa maeneo husika katika  ujenzi wa barabara inayopita Arusha ya kilomita 42.4 pamoja na uekaji wa alama za barabarani pembeni ya barabara zote mbili.

Kenia Wahlen Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru KenyattaPicha: Getty Images

Mabali na hilo mradi huo utakarabati kipande cha barabara ya Mtetwa-Taveta nchini Kenya ambacho kina ukubwa wa kilomita 89  pamoja na kipande cha barabara ya kupitaia Taveta cha kilomita12 na hudumna zote za barabarani katika eno la Bura,na Maktau katika barabara ya Mwatate-Taveta nchini Kenya.

Barabara ya Arusha-Holila na Taveta-Voi ni moja ya Chemba  muhimu ya usafiri katika Kanda ya Afrika Maashariki ikiwa na lengo  la kuimarisha na kurahisisha shuguli za kibaishara na kuongeza ushindani wa kimasoko wa kanda hiyo katika masoko ya kimataiafa na kuweka muingiliano mzuri katika ya nchi hizo.

Endapo mradi huo wa barabara utakamilika,utaunganisha bandari ya Mombasa upande wa kaskazini na Kaskazini ya Mashariki ya Tanzania na nchi zisizokuwa na bandari za Burundi, Rwanda, DRC  na Uganda na kuandaa njia mbadala ya baharini.

Benki ya Maendeleo ya Afrika ,ni taasisi ya maendeleo ambayo imeanzishwa kwa lengo la kuchangia katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi za Afrika,ambapo Benki hiyo inajumuisha vitengo vikuu vitatu,kitengo cha maendeleo cha Afrika AFDB, mfuko wa maendeleo wa Afrika ADF na mfuko wa udhamini wa Nigeria NTF.

Mwandishi:Hashim Gulana/  AFDB

Mhariri: Mohammed Khelef