Afisa wa zamani katika jeshi la Rwanda ahukumiwa miaka 20 jela
5 Julai 2007Matangazo
Mahakama ya Ubelgiji imemhukumu kifungo cha miaka 20 jela aliyekuwa afisa wa jeshi la Rwanda Meja Bernard Ntuyahaga baada ya kumkuta na hatia ya kuhusika na mauaji ya wanajeshi 10 wa Ubelgiji wa kulinda amani katika kipindi cha mwanzo cha mauaji ya mwaka 1994 nchini Rwanda.
Hata hivyo mahakama haikumkuta na hatia ya kuhusika na mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Rwanda wakati huo bibi Agathe Uwilingiyimana.
Bwana Bernard anaweza kukata rufaa kupinga hukumu hiyo