1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika ina idadi kubwa ya watu wanaougua COVID-19

Grace Kabogo
21 Mei 2021

Wagonjwa mahututi wanaougua COVID-19 barani Afrika, wako katika hatari kubwa ya kufa kuliko walioko katika mabara mengine, kutokana na ukosefu wa vifaa madhubuti vya kuwashughulikia wagonjwa hao.

https://p.dw.com/p/3ti4E
Beitbridge Grenzübergang zwischen Südafrika und Simbabwe
Picha: Guillem Sartorio/AFP/Getty Images

Taarifa hiyo ni kulingana na uchunguzi uliochapishwa siku ya Ijumaa. Bruce Biccard kutoka hospitali ya Groote Schuur na Chuo Kikuu cha Cape Town, Afrika Kusini aliyeuwongoza utafiti huo amesema, watu barani Afrika hawajaathirika vibaya na ugonjwa huo ikilinganishwa na maeneo mengine nje ya bara hilo, hasa linapokuja suala la idadi ya vifo na maambukizo.

Hata hivyo, idadi ya vifo vya wale walioambukizwa virusi vya corona huenda ikawa ya juu kuliko vile inavyoelezwa kufuatia ukosefu wa kukusanya data. 

Utafiti huo ulifanyika kwa kuwafuatilia wagonjwa 3,000 waliougua virusi vya corona waliolazwa katika vyumba mahututi katika mataifa 10 ya Afrika kati ya Mei na Desemba mwaka jana. Nusu ya wagonjwa hao walifariki ndani ya siku 30 baada ya kulazwa hospitalini. 

(AFP)