1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

Afrika: Wataalamu wakubaliana kuimarisha mifumo ya kodi

31 Agosti 2023

Kongamano la watafiti wa masuala ya kodi kutoka nchi zaidi ya 40 Afrika limehitimishwa leo na kuazimia masuala kadhaa ikiwamo kuwa na sera na sheria zitakazowezesha ukusanyaji wa mapato kutoka sekta isiyo rasmi.

https://p.dw.com/p/4Vop2
US-Dollars und Ägyptisches Pfund
Picha: Khaled Elfiqi/epa/dpa/picture alliance

Hayo yameelezwa leo na watafiti waliowasilisha tafiti mbalimbali za kikodi na kisha Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipa kodi wa mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) Richard Kayombo  alikuwa na haya ya kusema.

Muhtasari wa taarifa ya tathmini ya sekta isiyo rasmi nchini Tanzania wa mwaka 2018 unabainisha kuwa sekta isiyo rasmi katika shughuli za kiuchumi nchini Tanzania ni asilimia 92.8.

Tathmini hiyo inaonesha kwamba mjini ni asilimia 30.8 na vijijini ni asilimia 60.

Watafiti hao wamesema, Afrika  bado haina uzoefu wa kutosha katika ukusanyaji wa kodi ya mapato hususani kwenye Taasisi za kimataifa.

Soma piaWatafiti wa kodi barani Afrika wakutana Tanzania
Akizungumza wakati akifunga kongamano hilo, Kamishna wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA) Alphayo Kidata amesema nchi za Afika zinahitaji suluhisho la kudumu la ukusanyaji kodi wenye tija

Amesisitiza kuwepo kwa uwazi na uwajibikaji katika sekta za kodi Afrika ili mapato hayo yatumike katika elimu, afya na huduma nyingine za jamii.

Kuzibwe mianya ya upotevu wa mapato

Kuhusu upotevu wa mapato yatokanayo na kodi Afrika, Mtaalamu wa masuala ya uchumi na kodi Tanzania, Profesa Ibrahim Bakar ameshauri taasisi zilizojukumu na kukusanya kodi kuwajibika kwa dhati.

 Soma pia:Tanzania kupoteza mapato ya bilioni 100 kutokana na vita Ukraine
Mkutano huo ulioanza juzi Agosti 29, ulijumuisha  pia utolewaji wa tuzo kwa tafiti bora za masuala ya kodi ambapo watafiti watatu kutoka Togo na Malawi, walituzwa kwa kuwasilisha tafiti zenye tija.

Nchi zaidi ya 40 wanachama wa mtandao wa tafiti za kodi Afrika zilikutana na kuwasilisha tafiti hizo za masuala ya kodi kwa nchi za Afrika
 

Ni kwa nini Waafrika Kusini wageukia uchumi usio rasmi?