1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ahmadinejad aapishwa

5 Agosti 2009

Rais Ahmadinejad aanza awamu yake ya pili

https://p.dw.com/p/J3wO
Mahmoud Ahmadinejad

Rais Mahmoud Ahmadinejad ameapishwa rasmi Bungeni,mapema asubuhi ya leo kwa kipindi cha pilii cha miaka 4 kama raiis wa Iran.Kuapishwa kwake kuligubikwa na mashtaka yanayoendelea kutolewa juu ya mizengwe iliopitishwa katika kuchaguliwa kwake hapo juni 12.

Kikosi kikubwa cha polisi na wanamgambo wa kujitolea wa kikosi cha Basij waliweka ulinzi mkali kandon mwa barabara zilizolizunguka Bunge la Iran,mjini Teheran ili kuzuwia fujo lolote dhidi ya kuapishwa kwa rais Ahmadinejad.

Katika hotuba yake ya kutawazwa kwa kipindi cha pili, rais Ahmadinejad alziambia nchi za magharibi ambazo hadii sasa zimekataa kumpongeza kwa kuchaguliwa kwake :

"Hakuna yeyote nchini Iran anaesubiri pongezi kutoka kwenu."

Viongozi wa dola nyingi za kambi ya magharibi pamoja nazo uingereza,Ufaransa na Ujerumani, wamekataa kumpongeza rais Ahmadinejad kutokana na tuhuma za udanganyifu unaodaiwa kupitishwa katika kuchaguliwa kwake kwa muujibu Upinzanii nchinii unavyodaii. Wiimbi la malalamiko lilifuatia tangazo la ushiindii wake ambamo zaidii ya watu 20 waliuwawa .Zaidi ya wakosoajii wa serkali 1000 wakatiwa korokoroni na zaidi ya 100 kati yao bado wamo gerezani.

Ahmadinejad amesema dola za magharibi zimecheza kamari na kupoteza uaminifu wao zilipojiingiza wazi katika utaratibu wa uchaguzi nchini Iran.

Akiutetea msimamo wa nchi za maghariibi hivi majuzi, raiis barck Obama wa Marekani alisema:

"Tulichotaka tumekipata-yaani kutoa taarifa ya mshikamano kulaani viikali vile waandamanaji wa amani walivyoandamwa baada ya uchaguzi wa Iran pamoja na vitendo vilivyokiuka desturi za kimsingi za kimataifa-mfano kuzivamia afisii za kiibalozi,kuwakamata watumishi wek na kuwawekewa vizuwizi waandiishi habari."

Wakati akionesha kutojalii malalamiko yanayoendelea kutolewa dhidi yake, rais Ahmadinejad alisema kushiiriki kwa umma mkubwa katiika uchaguzi ule wa rais ni kuyatambua mapinduzi ya kiislamu ya 1979 pamoja na mkondo wa kisiasa iliofuata Iran mnamo maka 4 iliopita.

Akasema si muhimu nani alimtilia kura nani bali muhimu sasa,aliongeza, ni kuonesha uzalendo wa kitaifa na mkono kwa mkono kupiga hatua moja kubwa kuelekea usoni kuleta mabadiiliko mapya.Rais Ahmadinejad akasema kwamba katika kipindi cha pili cha uongozi wake ,Iran itasimama kidete zaidi dhidi ya kambi ya magharibi na haiatapiga magoti kuitikia vishindo inavyoitia Iran.

Hapo awali, rais Ahmadinejad alisema kuwa Iran itabakia tu kuzungumza na Shirika la Nguvu za Atomiki Ulimwenguni (IAEA) na haitajadiiliana tena na wanachama 5 wa kudumu wa baraza la Usalama la UM pamoja na Ujerumani kuhusu mradi wake wa kutatanisha wa kinuklia.

Rais Ahmadinejad sasa ana wiki 2 kuunda na kutangaza Baraza lake la mawaziri baada ya kuapiishwa hii leo Bungeni.Atapaswa kulikabidhi Bunge kuliidhinisha.

Kwa muujibu wa mashahidi Uwanja wa BAHARESTAN mjini Teheran, ambako ndiipo Bunge lilipo, kulikuwapo maandamano ya hapa na pale nje ya Bunge hilo huku waandamanajii wakipaza sauti wakisema "Kifo kwa dikteta" na kumtuhumu rais huyo kupitisha mizengwe.

Polisi yabainika walitumia hewa ya pilipili ya kutoa machozi ili kuwatawanya wapinzani hao na wakazidisha ulinzi kabla rais Ahmadinejad kukariibua kuondoka Bungeni.Kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi wa rais wa Juni 12, waandiishi habarii wa kigeni walialikwa na serikali kuripotii sherehe ya asubuhi ya leo ya kuapishwa rais Ahmadinejad.

Mwandishi:Ramadhan Ali/RTRE

Mhariri:M.Abdul-Rahman