1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Algeria: Miaka 60 tangu majaribio ya nyuklia ya Ufaransa

Ibrahim Swaibu Mhariri: Zainab Aziz
13 Februari 2020

Ni miaka 60 sasa  tangu Ufaransa ilipofanya majaribio yake ya kwanza ya bomu la nyuklia nchini Algeria, majaribio hayo yalisababisha madhara makubwa.Wahanga bado wanadai fidia kutoka kwa serikali ya Ufaransa.

https://p.dw.com/p/3Xjva
Algerien | Französische Atomtest in der Wüste von Reggane
Picha: Getty Images/AFP

Februari 13 daima itakumbukwa aliyekuwa fundi umeme, Jean-Claude Hervieux mwenye umri wa miaka 80 bado anakumbuka pale alipoungana na askari na maafisa wa ngazi za juu katika jangwa la Sahara nchini Algeria kushuhudia majaribio ya kwanza ya nyuklia yaliyofanywa na Ufaransa ameeleza kwamba mambo hayakuenda kama ilivyopangwa kwa sababu badala ya bomu hilo la nyuklia kubakia chini ardhini, vumbi na mionzi ya nyuklia pamoja na vipande vya mawe viliruka na kutapakaa angani. Kila mtu alikimbia, ikiwa ni pamoja na mawaziri wawili wa Ufaransa. Ufaransa ilikuwa nchi ya tatu kuwa na bomu la aina hiyo baada ya Marekani, Muungano wa Kisovieti (Urusi) na Uingreza,

Lakini hadi sasa bado wahanga wa majaribio hayo yaliyofanyika nchini Algeria karibu na mpaka wa Mauritania wakati wa utawala wa Ukoloni wa Ufaransa wananung'unika na kuitaka serikali ya Ufaransa iwalipe fidia kutokana na madhara waliyopata wakati wa jaribio hilo miaka sitini iliopita.

Mchambuzi wa wa masuala ya ukanda wa kaskazini mwa Afrika katika taasisi ya Mahusiano ya Kimataifa ya Paris Brahim Oumansour amesema hatua hiyo ni mojawapo hatua  ya  raia wa Algeria kulaani ukoloni na wakati huo huo wanataka Ufaransa ikiri uhalifu ilioufanya wakati wa utawala wake wa Kikoloni nchini humo. ' Oumansour amesema Ufaransa haiko tayari kukubali kwa sababu hilo litamaanisha kwamba taifa hilo litalipa fidia thamani ya mamilioni ya Euro.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel MacronPicha: AFP/G. Fuentes

Wiki iliyopita, akitoa hotuba inayohusu sera ya nyuklia, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron hakusema lolote kuhisiana mpango wa kuwafidia wahanga wa majaribio ya bomu la nyuklia nchini Algeria.

Kufikia sasa ni watu wachache tu ambao wamelipwa fidia na Ufaransa miongoni mwao akiwa raia mmoja wa Algeria. Tume ya fidia ya Ufaransa imeleeza kwamba imewalipa fidia watu waliotimiza vigezo kulingana na sheria.Wakosoaji wamesema huenda watu wengi zaidi waliathirika na majaribio hayo

Daktari mstaafu, Roland Desbordes raia wa Ufaransa anasema anazo kumbukumbu zinazoonyesha gesi chafu ikienea angani kutoka kwenye majabali baada kulipuliwa kwa mabomu. Daktari huyo ambaye kwa sasa ni msemaji wa kundi la utafiti kuhusu usalama wa mabomu ya atomic amesema jeshi la Ufaransa lina taarifa muhimu kuhusiana na jaribio la 1960 lakini limekataa kuzitoa. Pia zinaeleza kuhusu madhara makubwa kwa mazingira na afya kutokana na miripuko hiyo amesema serikali ya Algeria pia inabeba lawama na ameongeza  kusema serikali hiyo inabidi kuchukua hatua za kuyafunga maeneo ambapo majaribio hayo yalifanyika.

Wakati Ufaransa ikiadhinsha miaka sitini baada ya majaribio hayo, maswali yanazidi  kuongeza mvutano wa miaka nyingi  kati yake na Algeria.  Ufaransa iliripua zaidi ya vifaa 200 vya nyuklia nchini Algeria wakati wa majaribio yake hadi mwaka 1996 ambapo aliyekuwa rais wa Ufaransa Jacques Chirac aliposimamisha kufanya majaribio ya nyuklia.

Wanaharakati nchini Algeria wamesema maeneao yalikofanyika majaribio hayo bado yana gesi chafu ambazo zinaathiri afya ya binadamu lakini mamlaka haijaweka vizuizi  kuyatenganisha maeneo hayo na maeneo ya watu. Ripoti ya shirika la habari la Aljazeera inaeeleza kuwa kati ya watu 27,000 na 60,000  waliathirikia kutokana na majaribio hayo, tofauti na idadi inayo kadiriwa na Ufaransa na Algeria.

Chanzo: DW