1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS: Maafisa wa polisi wameuawa Algeria

5 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCML

Nchini Algeria,maafisa 5 wameuawa baada ya kituo cha polisi kuvamiwa katika eneo la Kabylei, mashariki ya mji mkuu Algiers.Askari polisi 3 pia walijeruhiwa katika shambulio hilo,ikidhaniwa kuwa limefanywa na wanamgambo wenye itikadi kali za Kiislamu.Kituo hicho cha polisi kilishambuliwa kwa risasi na gruneti zilizorushwa kwa makombora. Wanamgambo na polisi walifyatuliana risasi kwa muda wa saa mbili.