1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ALGIERS: Mripuko wa bomu umeua 3 Algeria

15 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBPl

Polisi nchini Algeria imesema,watu 3 wameuawa na wengine 5 wamejeruhiwa,baada ya bomu lililotengenezwa kienyeji,kuripuka mbele ya kituo cha polisi katika mji wa Zemmouri,ulio kama kilomita 50 kutoka Algiers.Hakuna aliedai kuhusika na shambulizi hilo.

Juma lililopita mashambulizi mawili ya bomu yaliua zaidi ya watu 50 nchini Algeria.Tawi la mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda nchini Algeria, limedai kuwa limehusika na mashambulizi hayo.