1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AMURIA:Misaada ya dharura yahitajika kwasababu ya mafuriko

22 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNd

Mashirika ya misaada yanatoa wito wa kupewa msaada wa mamilioni ya fedha ili kuwasaidia zaidi ya watu milioni 1 barani Afrika wanaokumbwa na mafuriko.Mafuriko hayo yamesababisha vifo vya watu takriban 200 na maelfu ya wengine kuachwa bila makao katika mataifa 17 yakiwemo Burkina Faso,Ghana, magharibi ya Togo,Sudan,Uganda na Kenya.Umoja wa mataifa unatoa ombi la dola milioni 43 kwa nchi ya Uganda ambako watu 50 wamefariki aidha kuimarisha maisha ya wakazi walioathirika na mafuriko hayo.

Uholanzi inaahidi kutoa euro milioni 11.Sudan inapangiwa msaada wa euro milioni 7,Uganda milioni 2 na zitakazosalia zitapelekwa kwa mataifa mengine ya magharibi mwa Afrika kwa mujibu wa serikali ya Uholanzi.

Shirika la misaada la Msalaba Mwekundu linatangaza ombi la dharura la msaada na kutuma wataalam wa majanga barani Afrika ili kusaidia kuchangisha pesa za kutengeza nyumba na kununua vidonge vya kusafishia maji.