1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA:Abdula Gul ashindwa katika awamu ya pili ya uchaguzi

24 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBWK

Mgombea wa chama tawala cha Uturuki AKP Abdula Gul ameshindwa katika awamu ya pili ya uchaguzi wa rais unaofanywa na bunge la nchi hiyo.Waziri huyo wa mambo ya nje ni mswalihina na juhudi zake za mwanzo za kuwania nafasi hiyo zilisababisha mvutano nchini humo. Uchaguzi huo wa rais unafanyika kwa awamu nne.Kiongozi huyo huenda akapata ushindi katika awamu ya tatu iliyopangwa kufanyika Agosti 28 ambapo wingi wa wawakilishi tu ndio unaohitajika.

Shughuli hiyo itakamilisha mvutano wa kisiasa uliodumu kwa miezi minne kati ya wafuasi wa misingi isiyo ya kidini na chama tawala cha AKP nchini Uturuki.

Wafuasi hao wanapinga uteuzi wa Bwana Gul kwa kuhofia kuwa huenda ukadharau maadili yasiyo ya kidini yaliyopewa umuhimu katika katiba.Hata hivyo Bwana Gul yuko mstari wa mbele katika juhudi za kusukuma Uturuki kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Uteuzi wake mapema mwaka huu ulisababisha mkwamo wa kisiasa ambapo mamilioni ya wakazi wa Uturuki pamoja na jeshi waliandamana kuupinga.Jeshi la Uturuki limepindua serikali 4 tangu mwaka 60.