1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ARUSHA : Waasi wa Dafur wakutana kuondosha tofauti

4 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcP

Makundi ya waasi wa Sudan wanakutana katika mji wa Arusha nchini Tanzania kwa mazungumzo yenye lengo la kuondosha tafauti zao na kufikia msimamo wa pamoja kabla ya mazungumzo ya amani na serikali.

Mkutano huo umeitishwa na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kufuatia kuidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kikosi cha wanajeshi 26,000 kulinda amani huko Dafur.

Mkutano huo umefunguliwa rasmi jana usiku kwa taarifa fupi kufuatia mashauriano ya mchana na wawakilishi wachache wa waasi waliokuwa wamewasili.

Ni kundi moja tu la waasi wa Dafur kati ya matatu limesaini makubaliano ya amani na serikali.

Takriban watu 200,000 inaaminika kuwa wameuwawa na wengine milioni mbili kupotezewa makaazi yao tokea kuanza kwa mzozo huo zaidi ya miaka minne iliopita.