1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ASMARA: Viongozi wa upinzani wa Somalia watishia kupigana vita na jeshi la Ethiopia

13 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQJ

Viongozi wa upinzani wa Somalia wanaokutana mjini Asmara nchini Eritrea, wameunda muungano wa ukombozi wakitishia kupigana vita na wanajeshi wa Ethiopia walio nchini mwao katika hatua ambayo huenda ikazidisha hali ya wasiwasi kwenye eneo la pembe ya Afrika.

Muungano huo, umeundwa kufuatia makubaliano kati ya wajumbe takriban 400 wakiwemo viongozi wa kiislamu na maafisa wa zamani katika serikali ya Somalia na unaitwa Muungano wa ukombozi wa Somalia.

Mwaka jana wanajeshi wa Ethiopia walivuka mpaka na kuingia Somalia kuwasaidia wanajeshi wa serikali ya mpito ya Somalia kupambana na wanamgambo wa kiuslamu waliokuwa wakiudhibiti mji mkuu Mogadishu na eneo kubwa la kusini mwa Somalia kwa miezi sita.

Msemaji wa muungano huo, Zakariya Mahmoud Abdi, amesema lengo lao ni kuikomboa Somalia kupitia vita na juhudi za kidiplomasia.