1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Auschwitz - mahali penye historia ya kutisha

27 Januari 2022

Kambi ya mateso ya wayahudi ya Auschwitz iliyoko kusini mwa Poland imetembelewa na zaidi ya watu milioni 49 tangu ilipofunguliwa kwa ajili ya wageni mnamo mwaka 1947.

https://p.dw.com/p/4699C
Gedenkstelle Auschwitz  Birkenau Wachtürme
Picha: DW/M. Heuer

Kambi ya mateso ya wayahudi ya Auschwitz iliyoko kusini mwa Poland imetembelewa na zaidi ya watu milioni 49 tangu ilipofunguliwa kwa ajili ya wageni mnamo mwaka 1947. Kambi hiyo ambako mamilioni ya wayahudi waliouwawa enzi za utawala wa kinazi nchini Ujerumani, kawaida kila mwaka zaidi ya watu milioni 2 huitembelea wakitokea kila pembe ya dunia. Janga la Corona hata hivyo limeathiri pia kambi hiyo na wageni wanaoitembelea wamepungua.

Idadi ya wageni wanaoitembelea kambi ya mateso ya Auschwitz imepungua na kufikia kiasi watu 500,000 kwa mwaka. Kambi hiyo hadi mnamo mwaka 1945 ilikuwa iko kiasi kilomita 50 kutoka magharibi mwa mji wa Krakau,ikiwa ni eneo kubwa karibu na mji mdogo unaoitwa Oswiecim (Auschwitz). Hii leo kambi hiyo inapatikana katika jengo la makumbusho ya serikali pamoja na eneo la kumbukumbu la waliouwawa.

Konzentrationslager Auschwitz
Hili lango lina kumbukumbu yenye uchungu katika historiaPicha: picture-alliance/dpa/J. Woitas

Pamoja na kambi kuu tatu za mateso za wanazi,zilikuweko pia kambi nyingine  pembeni  za mateso zikiwa na mashine za kuendesha mauaji ya watu.Makumbusho iliyoko katika kambi kuu ya mateso ya Auschwitz peke yake na makumbusho ya kumbukumbu ya waliouwawa ya Birkenau hivi sasa ina ukubwa unaochukua hekari 191. Lakini nini hasa maana ya Auschwitz kwa mtazamo kihistoria na nani mwenye dhamana katika hatma ya baadae.

Soma pia: Miaka 75 tangu kambi ya Auschwitz ilipokombolewa

Auschwitz kwahakika huu ni mji mdogo huko Poland na mwanzoni kabisa kabla ya mji huo kujulikana kupitia kambi hiyo ya mateso ya wayahudi chini ya utawala wa wanazi nchini Ujerumani ukiitwa Oswiecim,mji mdogo uliopitia mambo mengi kihistoria.Uliwahi kuwa chini ya Austria na kisha ukawa chini ya kile kilichoitwa ufalme wa Bohemia au ile inayoitwa hivi sasa Jamhuri ya Czech lakini pia ikawahi kuweko mikononi mwa Austria kisha  Ujerumani na baade ukarudi tena mikononi mwa Poland.Baada ya kumalizika vita vya kwanza vya dunia mji huo ukawa tena ni sehemu ya Poland.

70 Jahre Befreiung KZ Auschwitz
Kemikali ya Zyklon B ilitumiwa kuwauwa wafungwaPicha: Frank Schumann/zb/picture alliance

Umaarufu wa mji huu wakati huo ulitokana na kuhitajika kwa maeneo ya kukaa wageni na wafanyakazi wa muda mfupi waliokuwa maeneo ya mkoa Upper Selesia ambao ni eneo kati ya Poland na Ujerumani na Bohemia au ile inayojulikana sasa kama Jamhuri ya Czech.Ulikuwa mji uliojengwa nyumba nzuri mpya za matofali na mbao. Ni makaazi hayo ambayo baadae yalikuja kugeuzwa na kuwa msingi wa kuanzishwa kambi za mateso na mauaji za Auschwitz.

Muda mfupi baada ya kuanza vita mnamo Septemba mwaka 1939 mji huo ulinyakuliwa kwa mabavu na Ujerumani na kugeuzwa haraka kuwa kambi ya mateso.

Soma pia: Karani wa kambi ya Kinazi apandishwa kizimbani

Baadae kambi hizo zikatanuliwa katika eneo kubwa zaidi na kupatikana kile kilichokuja kujulikana kama Auschwitz-Birkenau ikiwa ni Auschwitz nambari mbili kambi ambako yalifanyika mauaji ya wayahudi. Eneo hili linajulikana kutokana na histori ya picha zilizopigwa kutoka angani na vikosi vya wanaanga vya Marekani na Uingereza.

Auschwitz Fotoreportage 75 Jahre nach der Befreiung
Mamilioni ya Wayahudi waliuawa enzi za ManaziPicha: DW/M. Oliveto

Ifahamike kwamba kabla ya vita vya pili vya dunia  wakaazi 12,000 wa Auschwitz walikuwa ni wayahudi jamii hiyo ya wayahudi ilikuwa imeongeza kwa kasi katika eneo hilo kutokana na uhamiaji na idadi ya wajerumani asili ilikuwa imepunguwa kwa kiasi kikubwa sana katika vijiji vya eneo hilo. Hata hivyo hali hiyo ilibadilika baada ya Hitler kuishambulia Poland mnamo Septemba 1 mwaka 1939 na nchi hiyo kutwaliwa na jeshi.Wayahudi walilazimika kukimbia kupisha takasatakasa iliyofanywa na wanazi na eneo hilo kukaliwa na wajerumani.Waliondolewa kwa nguvu kwa nguvu na kupelekwa kwenye maeneo ya madongo poromoka na kama wapoland wengi walipelekwa kwa nguvu kwenda kufanyishwa kazi za dharubu.

Soma pia: Oskar Groening afungwa miaka minne jela

Wapoland wenye asili ya kiyahudi waliobakia katika eneo hilo waliishi katika maeneo ya msongamano na kutengwa kabisa na wajerumani katika mji huo na mnamo mwaka 1940 wengi walichukuliwa na kupelekwa vikosi vya Hitler katika makambi ya mateso au kupelekwa kwa nguvu kutumikishwa katika maeneo mengine na wachache waliobakia mnamo mwaka 1942 waliuliwa katika kambi za Auschwitz. Matumaini yaliyopo ni kwamba hatimae mwaka huu mnamo mwezi Aprili zitafanyika tena kumbukumbu zitakazohudhuriwa na walionusurika na kuoneshwa moja kwa moja kutoka kwenye eneo hilo.

Makala hii ilitafsiriwa kutoka kwa Kijerumani