1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Australia kuchagua bunge lao leo.

24 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSbx

Sydney. Wapiga kura nchini Australia wanakwenda kupiga kura kulichagua bunge jipya. Maoni ya hivi karibuni ya wapiga kura yanaonyesha kuwa chama cha Labour kinachoongozwa na Kevin Rudd kinaweza kuushinda muungano unaounda serikali wa Concervative Liberal unaoongozwa na waziri mkuu John Howard. Rudd ameahidi kutia saini mkataba wa ulinzi wa mazingira wa Kyoto na kuyaondoa majeshi yaliyobaki ya Australia kutoka Iraq. Howard ambaye amekuwa madarakani kwa muda wa miaka 11 iliyopita, amesema kuwa iwapo atashinda awamu ya tano ya utawala , atajiuzulu katika muda wa miaka miwili na kutoa madaraka kwa waziri wa fedha Peter Costello.