1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baada ya Ugiriki na Ureno sasa ni Uhispania

29 Aprili 2010

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini Berlin amekutana na wakuu wa taasisi za fedha kuujadili mgogoro wa fedha unaoikabili Ugiriki.

https://p.dw.com/p/N97z
Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) und der Präsident des Internationalen Währungsfonds (IWF), Dominique Strauss-Kahn, kommen am Mittwoch (28.04.2010) im Bundeskanzleramt in Berlin zu einem Statement für die Presse. Merkel traf die Vorsitzenden von fünf der wichtigsten internationalen Wirtschafts- und Finanzorganisationen zu Beratungen über die Wirtschaftskrise in Griechenland. Foto: Steffen Kugler/Bundesregierung dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel(kulia) na Rais wa IMF, Dominique Strauss-Kahn.Picha: picture-alliance/dpa

Baada ya kukutana na wakuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, Benki Kuu ya Ulaya na taasisi zingine za fedha mjini Berlin, kujadiliana njia ya kuisaidia Ugiriki inayokabiliwa na tatizo la madeni makubwa, Kansela Merkel alikariri kuwa Ujerumani itaisaidia Ugiriki lakini nchi hiyo pia inapaswa kuchua hatua zaidi.

Hata Mkuu wa IMF,Dominique Strauss-Kahn amesema, Ugiriki itapata msaada wa fedha lakini kilicho muhimu hivi sasa ni kuchukuliwa hatua za haraka. Amesema,uaminifu wa nchi za kanda inayotumia sarafu ya euro upo hatarini.

Inatathminiwa kuwa hadi mwaka 2012, IMF na nchi za kanda ya euro zitapaswa kutoa kati ya euro bilioni 120 na 135 kuisaidia Ugiriki.Ifikapo Mei 19,Ugiriki inapaswa kulipa deni la kiasi cha euro bilioni 9. Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya,Herman Van Rompuy ameitisha mkutano wa viongozi wa nchi za kanda ya Euro tarehe 10 Mei mjini Brussels.

European Council President Herman Van Rompuy speaks during a media conference at an EU summit in Brussels, Friday March 26, 2010. EU leaders hold the second day of a summit that so far has focused on Greek economic woes, with eurozone countries and the International Monetary Fund pledging financial support in a deal that aims to halt the government debt crisis undermining Europe's currency union. (AP Photo/Geert Vanden Wijngaert)
Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya,Herman Van Rompuy.Picha: AP

Mgogoro wa madeni sasa umeenea katika nchi zingine za Ulaya. Kwani baada ya Ugiriki na Ureno, sasa Uhispania pia imeorodheshwa na shirika la "Standard and Poor´s" kama ni nchi isiyo na uwezo wa kulipa madeni yake. Shirika hilo hutathmini uwezo wa nchi kulipa madeni yake.

Viwango vya riba viliongezeka siku ya Jumatano, baada ya Ugiriki na Ureno hapo awali kutiwa katika orodha ya nchi zisizoaminiwa kukopeshwa. Sasa Ugiriki inalazimika kutoa riba ya asilimia 12 ili kuweza kupata mikopo mipya katika masoko ya fedha. Hiyo ni mara nne zaidi kuliko ile inayolipwa na Ujerumani.

Mhariri:P.Martin/DPA