1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baba Mtakatifu azungumza na maaskofu.

Abdu Said Mtullya17 Februari 2010

Baba Mtakatifu alaani ulawiti.

https://p.dw.com/p/M3hD
Baba Mtakatifu Benedikt wa 16 amesema ulawiti ni dhambi kubwa kwa Mungu.Picha: picture-alliance / dpa

Baba Mtakatifu Benedikt wa   16 amelaani uhalifu wa kuwalawiti watoto wa kiume makanisani kuwa ni dhambi  dhidi ya mwenyezi Mungu.

Baba Mtakatifu ametoa  shutuma hizo baada ya kukutana  na maaskofu kwenye makao yake makuu  ya Vatican.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani ametoa kauli   hiyo kufuatia kufichuka kwa habari juu ya ufidhuli uliotendwa  na makasisi nchini Ireland wa kuwalawiti watoto. Baba Mtakatifu Benedikt wa16 amesema pamoja na kuwa vitendo vya kuchukiza, ufidhuli huo ni dhambi kubwa kwa  Mwenyezi Mungu.

Baba Mtakatifu amelaani kudhalilishwa kwa watoto wa kiume kingono kuwa siyo tu ni uhalifu, bali pia ni dhambi  kubwa kwa Mwenyezi Mungu.

Amesema vitendo hivyo vinakiuka hadhi ya mwanadamu alieumbwa kwa mfano wa Mungu.

Baba Mtakatifu amewataka maaskofu wa Ireland aliokutana nao kwa muda  wa  siku mbili wachukue hatua ili kurejesha  imani na uadilifu  wa kanisa.

Kanisa katoliki nchini  Ireland lilikumbwa na kashfa ya  watoto wa kiume kugeuzwa wanawake baada  ya tume iliyoongozwa na hakimu  Ynonne  Murphy  kulishutumu kanisa katoliki  nchini Ireland kwa kutoyazingatia  ipasavyo madai juu ya kutendeka kwa mikasa 300 ambapo  watoto wa kiume walilawitiwa.

Tume hiyo ilitoa lawama hizo mwezi novemba  mwaka jana kuhusiana  na madai ya kufanyika vitendo hivyo  katika dayosisi ya Dublin kati  ya mwaka 1975 na  2004.  

Makasisi  24  wa Ireland  walioitwa  na baba Mtakatifu  kujadili kashfa hiyo walimwambia kiongozi huyo   wa kanisa katoliki kuwa wametahayari juu ya kashfa hiyo na wameahidi  kushirikiana na kanisa.

Katika  tamko lao maaskofu  hao  wamesema hatua muhimu sasa zimechukuliwa  ili kuhakikisha usalama  wa watoto na vijana watakaohusiana na shughuli  za kanisa.

Mwandishi Mtullya/ZA AFPE

Mhariri: Miraji Othman