1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bafanabafana yachapwa na Uruguay

Aboubakary Jumaa Liongo17 Juni 2010

Wenyeji Afrika Kusini wamejiweka katika nafasi ngumu ya kufuzu kwa raudi ya pili ya fainali za kombe la dunia baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Uruguay.

https://p.dw.com/p/Nsqt
Diego Forlan akifunga bao la kwanza kwa Uruguay dhidi ya BafanabafanaPicha: AP

Alikuwa ni mshambuliaji wa Uruguay Diego Folan aliyepachika mabao mawili kabla ya Avaro Pereira kupachika la tatu na kuiweka Bafanabafana nchani mwa fainali hizo.

Bafanabafana ilishuhudia mlinda mlango wake Itumeleng Khune akipewa kadi nyekundu.Kipigo hicho kilizima kelele za vuvuzela na kutoa nafasi kwa washabiki wa Uruguay kuimba.

Mapema Uswis iliushangaza ulimwengu wa soka kwa kuwafunga mabingwa wa Ulaya Uhispania bao 1-0.Uhispani ni miongoni mwa timu ambazo zinapigiwa upatu kutwaa kombe hilo.

Mwandishi:Aboubakary Liongo