1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Al Maliki awakosoa makamanda wa Marekani

25 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCzN

Wizara ya mambo ya ndani ya Irak imetangaza kwamba watu wanne wameuwawa na wengine takriban 20 wakajeruhiwa leo mjini Bahgdad.

Majeshi ya Marekani na ya Irak yakisaidiwa na helikopta yamekabiliana na wanamgambo katika wilaya ya Sadr mjini Baghdad. Eneo hilo ni gome ya jeshi la Mahdi la shehe mwenye siasa kali, Moqtada al Sadr.

Taarifa ya jeshi imesema wanajeshi wa Irak na wa Marekani walifanya uvamizi ulioidhinishwa na serikali ya Irak kumkamata kiongozi wa wanamgambo anayeshukiwa kuongoza vikosi vya mauaji ya kikabila.

Lakini waziri mkuu wa Irak, Nouri al Maliki amesema hakushauriwa kabla ya shambulio hilo na amewakosoa vikali makanda wa jeshi la Marekani kwa kusema katika mkutano wao na waandishi habari leo kwamba Irak inahitaji kuweka tarehe ya kuzuia machafuko.