1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Hali ya raia inazidi kuzorota

11 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAh

Ripoti ya shirika la kimataifa la msalaba mwekundu imesema kwamba hali ya raia nchini Irak inazidi kuzorota.

Ripoti hiyo imesema kuwa ni vigumu kukadiria idadi halisi ya watu waliouwawa katika mashambulio ya risasi, mabomu au katika operesheni za kijeshi.

Muwakilishi wa shirika hilo la msalaba mwekundu Pierre Krähenbühl amesema.

Ijapokuwa ripoti hiyo imetaja kuwa kuna utulivu katika baadhi ya sehemu nchini Irak, imefahamisha kuwa wengi kati ya maafisa wa kutoa huduma za afya wanatoroka kutoka nchini humo siku hadi siku na idadi ya wakimbizi kutoka Irak imeongezeka.