1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Maandamano yapinga kukamatwa kwa Ammar al-Hakim

24 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOt

Mamia ya Wairaki wameandamana mjini Hillah,baada ya mtoto wa kiume wa mwanasiasa mashuhuri wa madhehebu ya Kishia,Abdul-Aziz al-Hakim kukamatwa na wanajeshi wa Kimarekani.Waandamanaji walikusanyika mbele ya ofisi za Baraza Kuu la Mapinduzi ya Kiiislamu la Irak mjini Hillah, kiasi ya kilomita 100 kusini mwa Baghdad.Ammar al-Hakim alikamatwa kwenye njia panda,kati ya Iran na Irak pamoja na walinzi wake siku ya Ijumaa na alizuiliwa saa kadhaa.Kwa mujibu wa wanajeshi wa Kimarekani,watu waliofuatana nae walisababisha wasiwasi.