1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Mabomu yanayotegwa kando ya barabara yanasabisha vifo vingi.

15 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2V

Bomu lililotegwa kando ya barabara ambalo lililengwa dhidi ya msafara wa maafisa wa serikali limesababisha vifo vya watu wanne waliokuwa karibu mjini Baghdad.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani amesema leo kuwa , maafisa hao ambao wanafanyakazi katika idara ya fedha ya wizara ya mambo ya ndani , walikuwa wanasafiri katika msafara lakini hawakuathirika.

Jana Jumamosi wanajeshi watatu wa Marekani wameuwawa kusini mwa Baghdad wakati gari yao ilipolipuliwa na bomu lililotegwa kando ya barabara.

Zaidi ya wanajeshi 40 wa jeshi la Marekani wameuwawa nchini Iraq mwezi huu. Wanajeshi wawili hadi watatu kwa wastani wanakufa kila siku nchini Iraq, wengi wakiwa ni kutokana na mabomu yanayotegwa kando ya barabara.

Wakati huo huo mwenyekiti wa chama cha pili kikubwa kwa upande wa Wasunni nchini Iraq amesema leo kuwa kugawanyika kwa nchi hiyo ni jambo ambalo halizuiliki iwapo mpango wa Washia wa kuwa na eneo lao upande wa kusini utafanikiwa.