1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Marekani na Iran kuzungumzia amani Iraq.

28 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxS

Marekani na Iran ziko tayari kumaliza miaka 27 ya kutokuwa na mahuasino katika ngazi ya juu ya kisiasa na kufanya mazungumzo kuhusu hali ya usalama ya Iraq.

Mkutano huo kati ya balozi wa Marekani nchini Iraq, Ryan Crocker na mwenzake wa Iran Hassan Kazemi , utafanyika mjini Baghdad leo Jumatatu.

Mpango ambao bado ni mchanga wa kinuklia nchini Iran hautakuwa katika ajenda ya mkutano huo.

Marekani inaishutumu Iran kwa kuchochea ghasia dhidi ya nchi hiyo jirani upande wa magharibi.

Wakati huo huo , Iran imerudia shutuma zake kuwa Marekani inaendesha mtandao wa kijasusi nchini Iran kama sehemu ya mkakati wa kuiangusha serikali ya Kiislamu nchini humo.

Marekani na Iran hazijakuwa na uhusiano rasmi wa kidiplomasia tangu mwaka 1980 baada ya kuachiliwa huru zaidi ya mateka 50 wa Kimarekani walioshikiliwa kwa muda wa siku 44 katika ubalozi wa Marekani mjini Tehran.