1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Marekani yathibitisha maiti ya askari wake.

24 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByt

Majeshi ya Marekani yamethibitisha maiti ilioopolewa kutoka mto wa Euphrates kusini mwa Baghdad ni ya mmoja miongoni mwa askari-jeshi watatu wa Marekani waliotoweka nchini Iraq.

Majeshi hayo yalianzisha msako mkali baada ya shambulio la tarehe kumi na mbili mwezi huu ambapo wanajeshi wanne na mtapta wao waliuawa.

Kundi lijiitalo Taifa la Kiislamu la Iraq ambalo lina uhusiano na mtandao wa al-Qaeda lilikuwa limedai linawashikilia wanajeshi hao.

Wakati huo huo, wanajeshi wawili wa Marekani wameuawa wakati wa harakati za kijeshi katika mkoa wa Anbar.