1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mkutano wa Irak kukomesha machafuko

8 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBY

Irak ikitafuta njia ya kukomesha machafuko nchini humo,itakuwa na mkutano wa usalama pamoja na majirani wake na madola makuu hapo tarehe 3 na 4 mwezi wa Mei katika mji wa mapumziko wa Sharm el Sheikh nchini Misri.Taarifa hiyo imetolewa na waziri wa masuala ya nje wa Irak,Hoshyar Zebari. Hapo awali,mkutano huo wa kilele,utakaoipa Marekani nafasi ya kuzungumza uso kwa uso pamoja na Iran na Syria,ulitazamiwa kufanywa mapema mwezi huu nchini Uturuki.