1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Mmuagiko wa damu unaendelea nchini Irak

20 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD15

Hadi watu 38 wameuawa na zaidi ya 140 wamejeruhiwa katika miji mbali mbali nchini Irak. Raia,polisi na wanajeshi wameuawa katika mashambulio ya mabomu ya gari,makombora na risasi zilizofyatuliwa katika miji ya Mosul,Kirkuk na Khalis.Jeshi la Kimarekani limesema linafikiria upya mkakati wake mjini Baghdad,baada ya vikosi vya Kimarekani vilivyoimarishwa katika mji huo kushindwa kuzuia mashambulio yanayozidi kufanywa na waasi na wanamgambo wa madhehebu mbali mbali.Kwa mujibu wa maafisa wa kijeshi wa Kimarekani,mashambulio mjini Baghdad yameongezeka kwa asilimia 22 katika kipindi cha majuma matatu yaliopita.