1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Rais Bush ahitaji muda kutuliza Baghdad

15 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRw

Jeshi la Marekani nchini Iraq limethibitisha kwamba wanajeshi wanne wa Marekani wameuwawa katika shambulio la bomu lililotegwa barabarani hapo jana katika jimbo la Dijala kaksazini mashariki kwa Baghdad.

Shambulio hilo limekuja wakati wanajeshi wa Iraq na Marekani wakiwa wameanzisha operesheni kubwa ya usalama katika mji mkuu huo kukomesha umwagaji damu.Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari hapo jana Rais George W. Bush wa Marekani amesema itachukuwa muda kuufanya mji wa Baghdad kuwa wa salama.

Rais Bush ametetea madai kwamba Kikosi cha Mapinduzi cha Iran kimekuwa kikiwapatia silaha wapiganaji wa Iraq hata hivyo amejitenganisha na matamshi yaliotolewa na maafisa wa serikali ya Marekani wasiotajwa majina kwamba maafisa waandamizi wa serikali ya Iran wameidhinisha usafirishaji huo wa silaha kwa wapiganaji hao nchini Iraq.