1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Shambulio la kujitolea muhanga limeua askaripolisi

11 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTF

Si chini ya askaripolisi 12 wameuawa na 40 wengine wamejeruhiwa katika shambulio la kujitolea muhanga lililofanywa mji wa Tikrit, alikotokea rais wa zamani wa Irak,marehemu Saddam Hussein. Maafisa wa polisi wamesema, mshambuliaji huyo aliripua lori la chakula cha mifugo lililojazwa miripuko.Shambulio hilo lilifanywa nje ya kituo cha polisi cha Ad-Dawr na jengo zima liliteketezwa.Wakati huo polisi wengi walikuwa wakienda kazini.